Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

TANZANIA NA CHINA KUIPA UHAI MPYA RELI YA TAZARA.


Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Samia Suluhu Hassan imeingia makubaliano na China kufufua na kuboresha reli ya TAZARA, hatua inayolenga kuimarisha uchumi wa kanda ya Kusini mwa Afrika.


Hatua hiyo inalenga kuipa uhai mpya miundombinu hiyo ya kihistoria iliyojengwa kati ya mwaka 1970 na 1975 kama kiungo muhimu cha kiuchumi kanda ya Kusini mwa Afrika.

Akizungumza katika kumbukumbu ya wataalamu 65 wa Kichina waliopoteza maisha wakati wa ujenzi wa reli hiyo , Waziri Patrobas Katambi alisema ushirikiano huo unaendeleza urithi wa kihistoria wa mataifa hayo.



Alieleza kuwa msingi wa ushirikiano huo uliwekwa na viongozi wa zamani akiwemo Julius Nyerere, Kenneth Kaunda na Mao Zedong.

Serikali imeahidi kuendeleza ushirikiano huo kupitia miradi mikubwa ya maendeleo, huku China ikiendelea kuwa mshirika muhimu katika kukuza uchumi na viwanda nchini..




Mwisho.


Post a Comment

0 Comments