Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

USALAMA KWANZA: JOGGING SOMANDA, WANANCHI WAKARIBISHWA KUKATA WESE.


Na marykitoto 

USALAMA Kwanza Jogging Club yenye maskani yake Somanda, ndani ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, inaendelea na maandalizi kuelekea kilele cha KATA WESE kinachotarajiwa kufanyika ndani ya mwezi wa nne.

Akizungumza leo na KITOTO DIGITAL wanachama wa klabu hiyo wamewahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kukata wese litakalofanyika kesho, Jumamosi. Lengo kuu ni kuimarisha afya ya mwili pamoja na kuendeleza mshikamano wa kijamii.

Katibu wa Wakata Wese, Norascus Usule, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika tukio hilo huku akiahidi burudani ya kutosha kwa washiriki wote. “Njoo ukate wese, burudani waachie sisi,” alisisitiza.


Kwa upande wake, Mkaguzi wa Kata ya Somanda, Insp. Mwinjuma Omary, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika juhudi za kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu, ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama wakati wote.

Kauli mbiu ya “Afya ni Mtaji” inaendelea kuwa chachu ya kuhamasisha wananchi kuthamini mazoezi ya mwili kama njia muhimu ya kuboresha afya na maisha kwa ujumla.


Wananchi wote wanakaribishwa kujumuika katika tukio hilo muhimu litakalojumuisha mazoezi, burudani na elimu ya usalama kwa jamii.

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments