Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

MUDATHIR YAHYA AFUNGIWA MECHI TATU, AKOSA DABI YA KARIAKOO MEI 3.

 


Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya, amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh1 milioni. Picha na Yanga

Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya, hatakuwepo katika kikosi cha timu yake kwenye pambano kubwa dhidi ya Simba litakalochezwa Mei 3, 2026, baada ya kufungiwa kufuatia adhabu ya kinidhamu.


Mudathir amepewa adhabu ya kufungiwa mechi tatu pamoja na kutozwa faini ya shilingi milioni 1 za Kitanzania. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubainika kuwa alimchezea vibaya kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji, Ibrahim Abraham, katika mchezo uliochezwa Aprili 8, 2026.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu ya msimu huu.


Kukosekana kwa Mudathir ni pigo kwa Yanga, hasa ikizingatiwa umuhimu wa mchezo huo dhidi ya watani wao wa jadi Simba, ambapo ushindani huwa mkubwa kila mara. Mashabiki sasa wanasubiri kuona jinsi timu itakavyojipanga kuziba pengo hilo muhimu katikati ya uwanja.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments