Na marykitoto
Mkazi wa Nyantorotoro B, Nyankumbu – Geita, Catherine Kachwele amezua gumzo baada ya kulazimika kumtelekeza mbuzi wake kwa zaidi ya miezi miwili kwa balozi wa shina, baada ya kubaini ana jinsia mbili—kiume na kike.
Catherine anasema alipokea mbuzi huyo kama malipo ya matibabu kutoka Kigoma bila kumkagua. Alipofika nyumbani, alishangazwa na umati wa watu waliovutiwa na mbuzi huyo, ndipo aligundua hali yake ya kipekee.
Baada ya taharuki na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali, aliamua kumwacha mbuzi huyo kwa balozi, akidai ni tukio la kwanza na la ajabu kuwahi kumtokea.
Wataalamu wa mifugo wanasema hali hiyo si ya kushangaza bali ni kasoro ya kuzaliwa (congenital anomaly), inayoweza kusababishwa na kuzaliana kwa mifugo wa ukoo mmoja.
Jamii imetakiwa kuachana na imani potofu na badala yake kupata elimu sahihi ya ufugaji ili kuepuka matukio kama hayo.
Mwisho.
0 Comments