Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

UKATILI WA PESA: MTOTO WA MIAKA 12 ACHOMWA MIKONO KISA CHA SHILINGI ELFU 5

Na marykitoto 



Mtoto wa kike, Abbi Nelson, mwenye umri wa miaka 12 na mkazi wa mtaa wa Kinyambi, kata ya Nkende, mjini Tarime, amepata majeraha makali mwilini baada ya kuchomwa na vifaa vinavyodaiwa kuwa vya umeme.


Tukio hilo limedaiwa kutokea pale ambapo mtoto huyo alichomwa mikono yote miwili, huku baba yake mzazi, Nelson, akimlazimisha kudai shilingi elfu tano kutoka kwa mtoto wake.


Tayari baba huyo amekamatwa na polisi kufuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Edward Gowele, kusimamia hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa kwa kitendo hiki cha ukatili.

Post a Comment

0 Comments