Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

TUKIO LA USHABIKI WA SIMBA NA YANGA LAGEUKA MAUAJI

 Na marykitoto 

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linaendelea na msako wa kumtafuta kijana mmoja (jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kumuua Abel Mazuri (25) na kujeruhi watu wawili kufuatia ugomvi uliotokana na ushabiki wa mpira kati ya timu za Simba na Yanga.

Tukio hilo limetokea Machi 24, 2026 majira ya saa 5:30 usiku katika kitongoji cha Nyamahengo, kijiji na kata ya Sumve, wilayani Kwimba mkoani Mwanza.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alimshambulia marehemu kwa kumchoma kifuani kwa kitu chenye ncha kali akiwa katika banda la kuoneshea mpira, kisha kuwajeruhi watu wengine wawili waliokuwepo eneo hilo wakinywa pombe na kuangalia mchezo.

Akizungumza Machi 25,2026,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbord Mutafungwa,amesema waliojeruhiwa ni Semen Cherehani (26) na Ndubu Chagula (26), wote wakazi wa kijiji cha Sumve, ambao walipata majeraha mikononi. Majeruhi hao wamepatiwa fomu za matibabu (PF3) na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Sumve, huku hali zao zikielezwa kuimarika.

uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ubishani uliotokana na ushabiki wa mpira uliovuka mipaka. Polisi wanaendelea na juhudi za kumkamata mtuhumiwa ili afikishwe ,Amesema Mutafungwa.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments