Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

SHINYANGA YATIKISA: MAFUTA AU MAJI? UCHUNGUZI MKALI UNAENDELEA KWA MAGARI YALIYOKUWA NA SHIDA.

 Na marykitoto 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), linafanya uchunguzi wa madai yanayohusiana na mafuta yaliyochanganywa na maji katika kituo kimoja cha mafuta mjini Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Janeth Magomi, ameeleza kuwa uchunguzi unafuata malalamiko ya wamiliki wanne wa magari waliodai magari yao kupoteza nguvu mara baada ya kujaza mafuta katika kituo hicho.

Wamiliki hao wanaamini kuwa mafuta waliyonunua huenda yalichanganywa na maji, jambo linalosababisha kushuka kwa utendaji wa magari yao. Uchunguzi wa pamoja na wataalamu wa EWURA unaendelea ili kubaini ukweli wa suala hili.

Kamanda Magomi amewataka wananchi kuwa watulivu na kusubiri matokeo ya kisayansi yatakayoeleza ukweli. Amesisitiza kuwa majibu sahihi yatatolewa baada ya uchunguzi wa kitaalamu .


Post a Comment

0 Comments