Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

MFUKO MAALUM WAZINDULIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAFUTA



Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi

Na Marykitoto 

Serikali imetangaza mpango wa kuanzisha Mfuko Maalumu utakaolenga kupunguza makali ya kupanda kwa bei ya mafuta, hali iliyochangiwa na mivutano ya kivita inayoendelea kati ya Israel, Marekani na Iran.

Akizungumza na vyombo vya habari Aprili 7, 2026, katika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amesema hatua hiyo inalenga kulinda uchumi wa wananchi dhidi ya athari za mabadiliko ya bei za kimataifa.

Kihongosi amesisitiza kuwa CCM kwa kushirikiana na Serikali itahakikisha upatikanaji wa mafuta unakuwa wa uhakika wakati wote, sambamba na kuhakikisha bei zinabaki nafuu kadri inavyowezekana.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali ina mpango wa kutoa ruzuku ya mafuta, kama ilivyofanya awali wakati wa vita kati ya Urusi na Ukraine, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 100 kilitolewa kusaidia kupunguza mzigo kwa wananchi.

Mwisho.


Post a Comment

0 Comments