Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

RC SONGWE ATOA KAULI NZITO... 'HAKUNA WIZI WA NYETI'


Na marykitoto

Mkuu wa mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame akizungumza na wananchi

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabir Omary Makame, amewataka wananchi kuacha kusambaza taarifa za uzushi zinazodai kuwepo kwa matukio ya watu kuibiwa sehemu zao za siri (nyeti).

Amesema taarifa hizo si za kweli na zina lengo la kuzua hofu na taharuki katika jamii. 

RC Makame amesisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufuatilia hali ya usalama mkoani humo, na hakuna tukio lililothibitishwa la aina hiyo.

Pia amewahimiza wananchi ,Kupuuza taarifa zisizo na uhakika Kutozisambaza kwenye mitandao ya kijamii na Kushirikiana na mamlaka kutoa taarifa sahihi

Kwa ujumla, ujumbe wake mkuu ni kutaka utulivu na kuzuia hofu isiyo na msingi miongoni mwa wananchi wa Songwe, hasa katika maeneo ya Tunduma.

Mwisho.

nini maoni yako kuhusu kisa hicho kilicho leta taharuki .  😆 

 




 

Post a Comment

0 Comments