Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

MAUAJI YA BODABODA DODOMA: WATU 3 WANASWA, PIKIPIKI YAPATIKANA.

 

Na marykitoto 

Hofu na simanzi imetanda jijini Dodoma kufuatia tukio la kusikitisha la mauaji ya dereva wa bodaboda, Omary Bakari (21), mkazi wa Michese, aliyeuawa kikatili kwa lengo la kunyang’anywa pikipiki yake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka , vijana watatu wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo la kinyama lililotokea usiku wa Machi 21, 2026 katika mtaa wa Chinyoya, kata ya Kilimani.

Inaelezwa kuwa marehemu alivamiwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mgongoni—kitendo kilichosababisha kifo chake papo hapo. Lengo kuu la washambuliaji hao lilikuwa kupora pikipiki yake.


Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 1, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, , alithibitisha tukio hilo na kueleza hatua zilizochukuliwa mara baada ya uhalifu huo.


Baada ya tukio, polisi walianzisha msako mkali uliofanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa mmoja, Sadick Jonathan (23), katika kijiji cha Mazase, wilayani Chamwino.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na pikipiki ya marehemu:

Namba: MC 556 FPE

Aina: Sinoray

Rangi: Nyeusi

Kwa mujibu wa Kamanda Hyera, mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na mauaji hayo, akiwataja wenzake wawili—Paulo Abiel (26) na Ramadhani Hamidu (35)—ambao walikamatwa baadaye walipokuwa wakijaribu kutorokea mikoa jirani.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments