Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

POLISI SIMIYU WAMEWAPA TABASAMU WANAFUNZI WENYE UHITAJI BARIADI MJINI, WAKILENGA KUIMARISHA ELIMU YAO.


Na marykitoto

JESHI la Polisi Mkoani Simiyu, limetoa misaada ya mahitaji kwa wanafunzi wenye Uhitaji katika Shule za Msingi Sima A na B zilizopo Halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani humo.

Zoezi hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Simalimeongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP), Edith swebe ambaye alishiriki katika tukio hilo lililokuwa limeandaliwa na Umoja wa Polisi Wanaume Mkoa wa Simiyu (UPW).

Kamanda Swebe amesema kuwa matendo hayo ya kujitolea yamelenga kutoa msaada kwa kuyafikia makundi mbalimbali yenye uhitaji maalum ambapo kwa mara ya kwanza umoja huo umeanza kwa Shule hizo za Msingi Sima A na B.

Kwa upande wa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Sunday Songwe amesema ameamua kuja na wazo hilo la kuanzia Umoja wa Polisi Wanaume (UPW) hii ni mara baada ya kuwepo na Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF Nets) ambao unalenga kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii.

Aidha, amesema lengo ya majitoleo hayo ni kurudisha tabasamu kwa kuwapatia kile ambacho walikuwa wanatamani kuwa nacho kama watoto wengine, kuwaongezea uwezo wa kufanya vizuri katika masomo na kutambua na kuunga mkono jitahada za Serikali za kuinua watoto kielimu hususani walio na upungufu wa mahitaji muhimu, ambapo zoezi hilo kwa mara ya kwanza limefikia zaidi ya Wanafunzi 600.

Kwa upande wa Afisa Elimu Msingi, Halimashauri Mji Bariadi, Mwl. Panta Theophacy amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kupitia Umoja wa Polisi Wanaume Mkoani humo kwa kufanya matendo ya majitoleo kitendo ambacho ni cha kipekee kabisa katika jamii, lakini pia hii inapelekea kujenga uhusiano wa karibu baina ya jamii na Jeshi la Polisi.

Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Msingi Sima A Mawazo Masanja ametoa shukurani za dhati kwa Umoja wa Polisi Wanaume Mkoa wa Simiyu kwa kuona umuhimu wa kuwafikia Wanafunzi wa Shule hizo za Sima A na B kwa kuwapa tia vifaa mbalimbali kama Sketi, Shati, Kaptula na Viatu kwa wale wenye uhitaji.

Aidha, amesema matendo hayo ya majitoleo yatarudisha faraja kwa Wanafunzi hao na kujiona na wao wapo sawa kama watoto wengine na itapelekea kuzidisha mahudhurio mazuri kwao.

Mwisho. 






Post a Comment

0 Comments