Na marykitoto.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anamringi Macha, tarehe 29 Aprili 2026 amekutana na watumishi wapya walioajiriwa katika Halmashauri za Wilaya ya Bariadi na kuwataka kuzingatia uzalendo, uwajibikaji na maadili ya utumishi wa umma.
Akizungumza katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Macha alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana, akibainisha kuwa zaidi ya watumishi 200 wameajiriwa Bariadi ndani ya mwaka mmoja.
mkuu wa Mkoa wa simiyu Mhe.Macha.
Alisisitiza kuwa shukrani kwa serikali zinapaswa kuonekana kwa vitendo kupitia utendaji kazi bora, huku akiwataka watumishi hao kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi ili kudumu katika ajira zao.
Aidha, aliwataka kuwa kiungo kati ya serikali na wananchi, na kuonya dhidi ya vitendo vinavyoweza kuleta mgawanyiko. Pia aliwahakikishia kuwa serikali ya mkoa itawaongoza na kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mwisho.
0 Comments