Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

DC SIMALENGA AZINDUA RASMI ZOEZI LA NIDA VIJIJINI; SERIKALI YASOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI.

 

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Simon Simalenga (kushoto) akishiriki kuona namna ya usajili wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) ilivyokuwa unafanyika katika kijiji cha Ikungulyabashahi wilayani Bariadi

Na marykitoto 

Bariadi, Mei 4, 2026 — Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga, amezindua rasmi zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),vijijini (Ikungulyabashahi) akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo muhimu.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Simalenga alisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kuwa na kitambulisho cha Taifa, akieleza kuwa ni nyenzo muhimu katika utambuzi wa uraia na upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.


Aidha, aliwataka wananchi kushirikiana na mamlaka husika kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini watu wasio raia wa Tanzania wanaojaribu kujipenyeza katika zoezi hilo.




Kwa upande wake, Afisa Usajili wa Mkoa, Ohana Ngotolainyo, alisema zoezi hilo lilianza rasmi Aprili 24, 2026, na linatarajiwa kukamilika Mei 20, 2026. Alisisitiza kuwa wananchi wote wanaostahili wanapaswa kutumia fursa hiyo kabla ya muda wa zoezi kuisha.




Katika hatua nyingine, baadhi ya wananchi wa Ikungulyabashahi  yohana misese na bi aisha ramadhani  wameipongeza serikali kwa kusogeza huduma hiyo karibu zaidi na makazi yao.

  "Walisema awali walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo, hali iliyokuwa ikiwanyima fursa ya kupata vitambulisho vya Taifa kwa wakati".




Zoezi hilo linatarajiwa kusaidia kuongeza idadi ya Watanzania wenye vitambulisho vya Taifa, hatua ambayo ni muhimu katika kuimarisha mifumo ya utambuzi wa raia na utoaji wa huduma bora nchini.

Mwisho.




Post a Comment

0 Comments