Na marykitoto
Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wanatarajiwa kushiriki kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya wazimamoto Duniani yatakayofanyika tarehe 4 Mei 2026 katika Wilaya ya Bariadi. Hafla hiyo itafanyika katika Kiwanja cha Sabasaba (CCM), ambapo shughuli mbalimbali zitaandaliwa kwa ajili ya kuelimisha na kuburudisha jamii.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya tukio hilo, Mrakibu msaidizi wa Zimamoto Faustin Mtitu ambaye ni kaimu Kamanda mkoa wa Simiyu anawakaribisha wananchi wote kuhudhuria kwa wingi ili kupata elimu juu ya masuala ya usalama wa moto na uokoaji.
Mbali na elimu hiyo muhimu, maadhimisho hayo yataambatana na michezo mbalimbali pamoja na burudani, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na jamii.
Siku ya wazimamoto Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 4 Mei, ikiwa ni fursa ya kutambua mchango mkubwa wa askari wa zimamoto katika kuokoa maisha na mali za wananchi, pamoja na kuongeza uelewa wa tahadhari dhidi ya majanga ya moto.
Wananchi wote wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki siku hii muhimu.
Mwisho.

0 Comments