Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

MITANDAO YA KIJAMII, UCHUMI NA MAHUSIANO: MZIZI WA TATIZO LA AFYA YA AKILI KWA VIJANA.

 

Baadhi ya vijana walioshiriki katika kongamano la la uzinduzi wa kampeni ya 'Kijana Tubonge', ambayo imelenga kuwaleta pamoja vijana wa kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35 kuwapa elimu itakayowasaidia kuongeza utambuzi juu ya umuhimu wa kulinda afya ya akili

Na mwandishi wetu.

Matumizi kupita kiasi ya mitandao ya kijamii, hali ngumu ya kiuchumi, changamoto za mahusiano ya kimapenzi, kushuka kwa ufaulu wa masomo, shinikizo la maisha pamoja na matarajio makubwa, na athari za mabadiliko ya tabianchi—yote haya yametajwa kuwa miongoni mwa vichocheo vikuu vya matatizo ya afya ya akili kwa vijana nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa Mei 1, 2026 na wadau mbalimbali wa afya ya akili wakati wa kongamano la uzinduzi wa kampeni ya “Kijana Tubonge”, inayolenga kuwakutanisha vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 35 na kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa kulinda na kutunza afya ya akili.

Kampeni hiyo imezinduliwa katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza uelewa na kupunguza unyanyapaa unaohusiana na masuala ya afya ya akili miongoni mwa vijana.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa taasisi ya Activista Tanzania, Edward Masele, amesema kuwa utafiti mdogo uliofanywa na taasisi hiyo umebaini kuwa changamoto hizo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa baadhi ya vijana kujikuta wakikumbwa na matatizo ya afya ya akili.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu, kujenga mazingira rafiki ya majadiliano, na kuwahamasisha vijana kuzungumza wazi kuhusu changamoto wanazokutana nazo ili kupata msaada mapema.
Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments