Pichani ni Mwili wa Restituta Moshiro (40) mkazi wa Mtaa wa Mnazi, Kata ya Ng’ambo mkoani Kilimanjaro ukiingizwa kwenye gari la polisi.
Na marykitoto
Usiku wa kuamkia Aprili 17 umeacha majonzi makubwa kwa wakazi wa Moshi, baada ya kuuawa kwa mama lishe mmoja aliyekuwa akijitafutia riziki kwa bidii.
Restituta Moshiro (40), maarufu kama “Mama Baraka,” mkazi wa Mtaa wa Mnazi, Kata ya Ng’ambo mkoani Kilimanjaro, aliuawa na watu wasiojulikana alipokuwa akirejea nyumbani akitoka kazini. Marehemu alikuwa akiuza chakula kando ya barabara kuu ya Moshi–Arusha, eneo la Shaka Tours.
Mwili wake ulipatikana katika shamba la mahindi, ukiwa na dalili zinazoashiria alifanyiwa ukatili kabla ya kuuawa. Tukio hilo limeibua hofu na huzuni kubwa kwa jamii, hasa kwa wafanyabiashara wanaofanya kazi nyakati za usiku.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, huku wananchi wakihimizwa kushirikiana ili wahusika waweze kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
Mwisho.

0 Comments