Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

UHURU WA HABARI KIUCHUMI: MISA TANZANIA YAKUTANISHA WADAU MWANZA


Na marykitoto.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA Tanzania), Edwin Soko, amevitaka vyombo vya habari nchini kuendelea kuandika na kuripoti habari zinazochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku vikizingatia weledi, ukweli na taarifa zilizohakikiwa.


Soko ameyasema hayo Oktoba 12, 2026, wakati wa Kongamano la MISA TAN Wadau lililofanyika jijini Mwanza, lenye kaulimbiu ya “Uhuru wa Vyombo vya Habari Kiuchumi,” lililowakutanisha wanachama 60 wa MISA Tanzania kutoka Kanda ya Ziwa, Magharibi na Kati pamoja na wadau kutoka taasisi za serikali na sekta binafsi.

Akizungumza katika kongamano hilo, Soko alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kutekeleza wajibu wake kwa jamii kwa kuzingatia misingi ya taaluma na kuchangia maendeleo ya taifa.

“Vyombo vya habari vinapaswa kuendelea kuandika na kuripoti habari zinazochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku vikizingatia weledi, ukweli na taarifa zilizohakikiwa.”


Kongamano hilo lilifunguliwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Daniel Machunda, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni.

Machunda aliye wasilisha salamu kwa niaba ya mgeni rasim, ameipongeza MISA Tanzania kwa kuwakutanisha wadau hao na kusisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuendelea kubaini na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo.

"Ushirikiano Kati ya waandishi wa habari na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kuifikishia jamii taarifa zenye manufaa kuongeza kuelewa wa wananchi na kuibua fursa zinazoweza kuchangia maendeleo ya uchumi" amesema machunda.




Wawakilishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) walizungumzia sheria na adhabu zinazohusiana na matumizi mabaya ya fedha, huku PSSSF ikiwasilisha historia ya kuanzishwa kwa mfuko huo na majukumu yake katika utoaji wa huduma za hifadhi ya jamii kwa wanachama.




Kwa upande wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA),  ilishiriki katika jukwaa hilo la wadau, inesema kazi yao kubwa ni kulinda na kusimamamia  haki  kwa kusimamia miongozo mbalimbali,huku TASHICO ikiwasilisha mafanikio yake, majukumu na mikakati ya mwaka wa fedha 2026/2027.




Kupitia kongamano hilo, wadau walipata nafasi ya kubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kuimarisha mawasiliano kati ya taasisi na vyombo vya habari ili wananchi waweze kupata taarifa sahihi kuhusu huduma na fursa mbalimbali za maendeleo.




Kaulimbiu ya kongamano hilo, “Uhuru wa Vyombo vya Habari Kiuchumi,” imeweka msisitizo katika mjadala wa umuhimu wa kuimarisha uwezo wa vyombo vya habari kujiendesha kiuchumi huku vikiendelea kulinda weledi na misingi ya taaluma.

Mwisho.







Post a Comment

0 Comments