Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

POLISI SIMIYU WATOA ONYO KWA WANAOFUMBIA MACHO WAHALIFU.



Na Kitoto Digital .

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Chacha Maro, amewataka wananchi kuacha tabia ya kufumbia macho wahalifu na badala yake kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya usalama ili kudhibiti vitendo vya uhalifu, hususan vinavyohusisha matumizi ya silaha.


Maro ametoa wito huo Oktoba 12, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanzoya, akiwahimiza kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi kwa kutoa taarifa kuhusu watu wanaowatilia shaka kuwa na viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.


Amesema ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama ni muhimu katika kuzuia uhalifu kabla haujasababisha madhara kwa jamii.



“Wananchi wanapaswa kuwa na utamaduni wa kutoa taarifa mapema wanapoona viashiria vya uhalifu ili hatua stahiki zichukuliwe kabla hali haijawa mbaya,” amesema Maro.



Aidha, amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya Watanzania wote, hivyo wananchi wanapaswa kutoa taarifa za matukio ya uhalifu katika vituo vya polisi ili sheria ichukue mkondo wake.



Ameongeza kuwa ushirikiano wa wananchi na Jeshi la Polisi utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao na kulinda maisha pamoja na mali za wananchi.

Mwisho.



Post a Comment

0 Comments