Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

🏆 MILIONI 13 KUIBUA VIPAJI KADOGOSA CUP 2026.

 


Na marykitoto. 

Mbunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini, Masanja Kungu Kadogosa, Juni 3,2026 ametoa jezi na mpira kwa timu zote 84 za vijiji zitakazoshiriki mashindano ya Kadogosa Cup 2026, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza vipaji vya vijana na kukuza michezo jimboni.



Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya mbunge, Mayala Shimji Lucas aliwataka viongozi wa kata kusimamia mashindano hayo kwa weledi ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Bariadi mhe. Mayala Lucas Diwani wa kata ya Kasoli 

Akitolea ufafanuzi juu ya mashindano hayo Mratibu wa Kadogosa cap yohana sitta alisema jumla ya Sh milioni 13.1 zitatolewa kama zawadi katika ngazi mbalimbali. Washindi wa kata 21 watapata Sh 200,000 kila mmoja, huku washindi wa ngazi ya tarafa wakijinyakulia hadi Sh 500,000.

Mratibu wa Kadogosa Cap 2026 Yohana Sitta 

 Katika fainali za ngazi ya jimbo, bingwa ataondoka na Sh milioni 3, kombe na medali 30, huku mshindi wa pili akipata Sh milioni 2 na mshindi  wa tatu Sh milioni 1.



Aidha, tuzo maalum zitatolewa kwa Mchezaji Bora, Mfungaji Bora, Golikipa Bora, Chipukizi Bora, Mwamuzi Bora pamoja na Timu Yenye Hamasa.


Baadhi ya vijana walioshiriki katika hafla ya uzinduzi huo wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini Masanja Kadogosa kwa kuandaa mashindano hayo, wakieleza kuwa yamekuwa chachu ya kuimarisha vipaji vyao, kuleta mshikamano miongoni mwao, na kuwapa fursa ya kujenga mahusiano bora ya kijamii pamoja na kujihusisha na shughuli za maendeleo zinazowainua kiuchumi na kijamii.




Kadogosa Cup 2026 inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuibua vipaji, kuimarisha mshikamano wa jamii na kuhamasisha maendeleo ya michezo katika Jimbo la Bariadi Vijijini. 🏆⚽

Mwisho. 

Na mpiga picha wetu khan kilunga .















Post a Comment

0 Comments