Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

SIMIYU YAPIGA VITA UHALIFU: POLISI WAVUNJA MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA NA NYARA HARAMU.

 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kupitia operesheni na misako mbalimbali inayofanyika katika maeneo tofauti ya mkoa huo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha Mei 1 hadi Mei 28, 2026, jumla ya watuhumiwa 85 wanaodaiwa kuhusika na makosa mbalimbali ya jinai walikamatwa.


Kati ya hao, watuhumiwa 60 wamefikishwa mahakamani na watuhumiwa 35 wamehukumiwa kutokana na makosa yao.
Katika operesheni hizo, watuhumiwa watano walikamatwa wakiwa na nyara za serikali bila kibali. 

Nyara hizo ni:
Nyama ya pori aina ya punda milia kilo 750
Nyama ya nyumbu kilo 505
Vipande vinne vya pembe za ndovu vyenye uzito wa kilo 16
Aidha, jumla ya kilo 140 za dawa za kulevya zilikamatwa, zikiwemo:
Mirungi kilo 50 (watuhumiwa 4)
Bhangi kilo 90 (watuhumiwa 5)
Pia, Mei 28, 2026 polisi waliteketeza shamba la bhangi lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja katika Kijiji cha Buhungukila, Wilaya ya Maswa, na kuwakamata watuhumiwa watatu.




Katika hatua nyingine, lita 120 za pombe haramu ya gongo zilikamatwa na watuhumiwa watano wanaodaiwa kujihusisha na utengenezaji na usambazaji wake.
Mei 21, 2026, watuhumiwa watatu waliokuwa walinzi wa kampuni binafsi walikamatwa kwa tuhuma za wizi wa gari aina ya Landcruiser Hardtop nyeupe yenye namba STM 6285 mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ametoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na uhalifu, huku akisisitiza kuwa operesheni zinaendelea. Pia amewahimiza wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu (RPC), Edith Swebe.

Katika kipindi cha Mei 1 hadi Mei 28, 2026, operesheni hizo zimeleta mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai, uteketezaji wa mashamba ya bhangi, pamoja na ukamataji wa nyara za serikali, dawa za kulevya na pombe haramu.

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu Chacha maro.

Jeshi la Polisi katika kuthibiti na kutokomeza kilimo cha bangi pamoja na biashara haramu ya dawa za kulevya. Tutapita katika kona zote za mkoa wetu wa Simiyu kuhakikisha tunakomesha kilimo hiki,” amesema chacha.

Watuhumiwa watatu waliokamatwa na jeshi la polisi wilaya ya Maswa ambayo wanadaiwa kulima zao la bangi katika kijiji cha Buhungukila.Pichani.


Hatua hizo zimekuwa sehemu ya juhudi za kudhibiti uhalifu na kuhakikisha jamii inaishi katika mazingira salama, huku Jeshi la Polisi likisisitiza ushirikiano wa wananchi katika kutoa taarifa za wahalifu na vitendo vya kihalifu kwa wakati.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments