Na marykitoto.
Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anamringi Macha, amesema kuwa ili mkoa uwe safi na wenye mazingira bora, jamii inapaswa kujenga desturi ya kudumu ya utunzaji wa mazingira kwani usafi ni jukumu la kila mwananchi.
Mhe. Macha amewataka wafugaji kuhakikisha wanatunza vyema mifugo yao na kuacha tabia ya kuiacha ikizagaa barabarani pamoja na maeneo yasiyoruhusiwa kuchungia, hali ambayo imekuwa ikichangia uharibifu wa miundombinu ya maendeleo.
mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi (mwenye kofia ya nembo ya Tanzania)
Aidha, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Ndugu Idd Ndabona, kuhakikisha zizi maalum linajengwa kwa ajili ya kuhifadhi mifugo yote itakayokuwa ikizagaa hovyo mjini.
Amesema mifugo hiyo itakamatwa na kuhifadhiwa hadi mmiliki atakapolipa faini, hatua ambayo imelenga kutoa onyo kwa wafugaji wote watakaokaidi agizo hilo.
Mhe. Macha amesisitiza kuwa marufuku hiyo ya kuzagaza mifugo itazingatiwa kwa siku zote za wiki isipokuwa siku ya Jumanne pekee, ambayo ni siku rasmi ya mnada.
Ametoa kauli hiyo Mei 16, 2026, wakati wa zoezi la usafi na utunzaji wa mazingira lililofanyika katika Halmashauri ya Mji Bariadi, wilayani Bariadi.
Mwisho.
0 Comments