Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

RC MACHA ARIDHISHWA NA MIUNDOMBINU YA MAJI MAONESHO YA NANENANE NYAKABINDI.



Na mwandishi wetu 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, amekagua miundombinu ya maji katika eneo la Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki yatakayofanyika katika eneo hilo.


Katika ukaguzi huo, Mhe. Macha ameridhishwa na utekelezaji wa miundombinu hiyo muhimu ya maji iliyowekwa kwa ajili ya kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa ufanisi wakati wa maonesho hayo makubwa ya kilimo na biashara.



Miundombinu hiyo imefungwa katika maeneo mbalimbali ya viwanja vya maonesho na kusimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bariadi (BARUWASA), hatua inayolenga kuboresha huduma kwa washiriki, wageni na wananchi watakaohudhuria maonesho hayo.



Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza BARUWASA kwa kazi nzuri ya kuhakikisha huduma muhimu ya maji inapatikana kwa wakati na viwango vinavyotakiwa, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kutunza miundombinu hiyo kwa manufaa ya wananchi na wageni wa Nanenane.


Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki yanatarajiwa kukutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na biashara kutoka maeneo tofauti ya kanda hiyo.

Mwisho.






Post a Comment

0 Comments