Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

ONYO NDOA ZA UTOTONI NA MATUMIZI YA FISI KWA WANAWAKE -DC SIMALENGA.





Na marykitoto

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe. Simon Simalenga  Mei 28, 2026 akiwa katika mkutano wa hadhara ulio hudhuliwa na mamia ya wananchi unaoendelea katika Kata ya Masewa, amesisitiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wa kike na wa kiume wanapata haki ya elimu bila ubaguzi. 


"Bado baadhi ya jamii zimeendelea kuwapeleka watoto shambani, kuwashirikisha katika shughuli za kuchunga mifugo pamoja na kuwaozesha watoto wa kike katika umri mdogo, hali inayochangia kudumaa kwa maendeleo ya watoto hao na taifa kwa ujumla ,Amesema Simalenga ".



Mhe. Simalenga amesema vitendo hivyo pia ni chanzo cha changamoto mbalimbali za kiafya na kijamii ikiwemo maambukizi ya magonjwa ya zinaa, HIV/AIDS, saratani ya mlango wa kizazi pamoja na ugonjwa wa fistula. 


Ameitaka jamii kubadilika kwa kuwapa watoto kipaumbele cha elimu na malezi bora ili kujenga kizazi chenye afya, maadili mema na uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa.



Aidha, katika mkutano huo, mkuu huyo wa wilaya aliwahimiza wazazi na walezi kuendelea kuchangia chakula shuleni. Alisema hatua hiyo ni muhimu katika kuboresha mazingira ya elimu na kuchangia ongezeko la mahudhurio na ufaulu wa wanafunzi.



Kwa upande wake, Afisa mwandambizi na kamanda Muhifadhi kutoka Pori la Akiba Kigereshi, Floravicky Kalambo, aliwataka wananchi hususan kina mama kuacha tabia ya kutumia fisi kama njia ya usafiri. 


Aliwasisitiza kuwa wanyama hao ni mali ya serikali na wanapaswa kuachwa waishi katika hifadhi kwa ajili ya uhifadhi wa maliasili na usalama wa mazingira.



Wananchi waliohudhuria mkutano huo walieleza kufurahishwa na ujio wa mkuu huyo wa wilaya, wakisema umeleta elimu muhimu kwa jamii. Pia waliunga mkono wito wa kuchangia chakula shuleni, wakibainisha kuwa mpango huo umesaidia kuongeza mahudhurio ya wanafunzi na kuboresha kiwango cha ufaulu shuleni.

Mwisho.


Na mpiga Picha wetu khan kilunga




Post a Comment

0 Comments