Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

KIHONGOSI APIGA MARUFUKU ADA YA SH600,000 KWA HOSTELI, WAZAZI WAPUMUA.

 

Katibu wa Itikadi  Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi (kulia) akihuhutubia mkutano wa hadhara mjini Musoma

Na mwandishi wetu 


Musoma, Mei 14, 2026 — Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amepiga marufuku utaratibu wa kuwatoza wanafunzi wa kidato cha nne Sh600,000 kwa ajili ya kukaa hosteli wakijiandaa na mitihani ya taifa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Musoma, Kihongosi alisema kiwango hicho cha fedha ni kikubwa na kinawaumiza wazazi pamoja na walezi wenye kipato cha chini.

Hatua hiyo inakuja baada ya taarifa kueleza kuwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makoko walitakiwa kulipa kiasi hicho ili waweze kupata huduma ya malazi ya hosteli kipindi cha maandalizi ya mitihani ya kitaifa.

Kihongosi alisisitiza kuwa elimu ni haki ya kila mtoto na hakuna mwanafunzi anayepaswa kunyimwa mazingira bora ya kujifunzia kutokana na gharama kubwa zinazowekwa na baadhi ya taasisi au shule.

Aidha, aliwataka viongozi wa elimu pamoja na mamlaka husika kufuatilia suala hilo haraka na kuhakikisha wanafunzi wanapata haki zao bila kuwepo kwa mzigo mkubwa wa kifedha kwa wazazi.

Wananchi waliohudhuria mkutano huo walionesha kuunga mkono kauli hiyo wakisema gharama za elimu zimekuwa changamoto kubwa kwa familia nyingi nchini
Mwisho.

Post a Comment

0 Comments