Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

🔥 BARIADI YACHANGAMKA! MKUU WA WILAYA SIMON SIMALENGA AONGOZA UZINDUZI WA CHANJO YA POLIO 💉

Na marykitoto 

Katika jitihada za kuimarisha afya ya watoto na kutokomeza ugonjwa wa polio nchini, Wilaya ya Bariadi imeanza rasmi zoezi la chanjo ya polio linalolenga watoto kuanzia umri wa siku sifuri hadi miaka 10. Zoezi hilo linafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 27 Machi, 2026






Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Wilaya, Simon Simalenga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, ambapo amewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote wanapatiwa chanjo hiyo ndani ya muda uliopangwa.

Pia amewataka Wakuu wa Wilaya na maafisa afya kusimamia kikamilifu zoezi hilo ili kuwafikia watoto wote, huku akishukuru ushirikiano wa wananchi waliojitokeza kwa wingi kushiriki uzinduzi huo.

“Tunataka tuhakikishe tunaondoa kabisa ugonjwa wa polio nchini,” alisema Simalenga.

Aidha, amekemea matumizi ya vyoo visivyo vya kisasa na kupinga upotoshaji wa taarifa kuhusu chanjo, akisisitiza utoaji wa elimu sahihi kwa jamii.

Wananchi kwa upande wao wameipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za afya, ikiwemo chanjo ya bure na huduma ya nyumba kwa nyumba.

Wataalamu wa afya wamesema chanjo ya polio ni salama na muhimu katika kuwalinda watoto dhidi ya ulemavu wa kudumu, huku wazazi wakihimizwa kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo hiyo.





Zoezi hilo linaendelea katika maeneo mbalimbali ya Bariadi na mkoa wa Simiyu ili kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa huduma hiyo muhimu.

##ChanjoYaPolio

#TokomezaPolio

#AfyaKwaWote

#PolioFree

#LindaMtoto

Post a Comment

0 Comments