Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

RC MTANDA, ASKOFU LYIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO SERIKALI NA KANISA

 


Na marykitoto.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda, amehakikishia kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa Katoliki katika kuimarisha huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya wananchi.


Mtanda ameyasema hayo Novemba 3, 2026, alipokutana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bariadi, Mhashamu Prosper Balthazar Lyimo, katika ofisi yake iliyopo Kanisa la Mtakatifu John, Somanda, Wilaya ya Bariadi.


"Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na Kanisa Katoliki katika sekta za elimu, afya, ustawi wa jamii na malezi ya kiroho. Ni muhimu kuendelea kushirikiana kwa karibu kati ya Serikali na viongozi wa dini ili kuleta maendeleo na mabadiliko chanya kwa wananchi."


Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za dini ni nyenzo muhimu katika kuimarisha maadili, mshikamano na ustawi wa jamii.


Kwa upande wake, Askofu Prosper Balthazar Lyimo, ambaye ni Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Bariadi lililoanzishwa mwaka huu, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa dhamira yake ya kuimarisha mahusiano na Kanisa.


"Kanisa Katoliki litaendelea kushirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo, kutoa huduma kwa wananchi na kuimarisha maadili katika jamii kwa manufaa ya waumini na wananchi wote."


Amesema ushirikiano huo utasaidia kuimarisha huduma za kijamii na kuchangia maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu.


Ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa Katoliki unatarajiwa kuendelea kuwa chachu ya maendeleo, amani na mshikamano katika jamii.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments