Na mwandishi wetu.
UONGOZI wa Kiwanda cha NIDA Textile Ltd, kilichopo Tabata- Dar es Salaam, umeipongeza Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kwa Usimamizi wake madhubuti wa zao la Pamba kuanzia maandalizi ya Mbegu, kupanda, kupulizia, kuvuna, kuhifadhi ghalani, kuuza viwandani, kuchakata marobota, kusafirisha mpaka kufika kiwandani hapo ikiwa katika Ubora huo huo.
Kiwanda hicho kinajihusisha na Utengenezaji wa nguo kutokana na malighafi ya zao la Pamba inayozalishwa nchini Tanzania huku Wasimizi wakubwa wakiwa ni Bodi ya Pamba.
Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho kilichopo Tabata, Dar es Salaam Muhammad Amin Godil, ambapo ameipongeza Bodi ya Pamba kwa kuongeza uzalishaji msimu hadi msimu.
Muhammad ametoa pongezi hizo baada ya kutembelewa na Maafisa kutoka TCB kwa lengo la kuona pamba ya Tanzania inavyotumika katika kiwanda hicho pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili kutokana na mnyororo wa zao hilo..
Aidha amoeonyesha kufurahishwa na kitendo cha maafisa hao kwenda kusikiliza changamoto zao kama wadau wakubwa wa mnyororo za zao la pamba huku akielezea changamoto ya Pamba inayozalishwa Tanzania wakati wa uchakataji nyuzi kukatika katika hali inayofanya ubora wa nyuzi kupungua na kupelekea soko kushuka.
Akitoa ufafanuzi katika changamoto hiyo mtaalamu wa Maabara na ubora wa pamba kutoka TCB, Bi Sharifa Salum amesema changamoto hiyo wakati mwingine inasababishwa na pamba kuvunwa kabla ya muda wake sahihi pamoja na changamoto ya kuathiriwa na hali ya Hewa .
Mwisho.







0 Comments