Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

CP ALEX MKAMA AWASILI SIMIYU KUIMARISHA POLISI JAMII NA USHIRIKIANO WA WANANCHI.

 

Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii, CP Alex Mkama.

Na marykitoto .

Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii, CP Alex Mkama, amewasili mkoani Simiyu leo Agosti 7,2026 kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Polisi Jamii pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi katika kudumisha amani na usalama.



Mara baada ya kuwasili, CP Mkama alipokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Edith Swebe, ambaye ni mwenyeji wake katika ziara hiyo.



Ziara hiyo ni sehemu ya ratiba ya kikazi ya Kamishna huyo katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwa na lengo la kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Polisi Jamii, kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi, wadau wa usalama na wananchi, pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu bora za kuimarisha ulinzi na usalama katika jamii.



Katika kipindi cha ziara hiyo, CP Mkama anatarajiwa kukutana na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa usalama ili kujadili mikakati ya kuendelea kuboresha dhana ya Polisi Jamii na kuongeza ushiriki wa wananchi katika kuzuia na kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Mwisho.





Post a Comment

0 Comments