Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

BAADA YA KM 8 ZA JOGGING, USALAMA KWANZA CLUB YAGEUKIA WAGONJWA BARIADI.

 

Usalama kwanza Jogging, kata wese "Afya ni mtaji".

Na marykitoto. 

Wanachama wa Usalama Kwanza Jogging Club wameadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho kwa kufanya jogging ya umbali wa kilomita 8, huku wakitumia fursa hiyo kurudisha kwa jamii kwa kuwafariji na kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Bariadi.



Zoezi hilo lililofanyika Julai 11, 2026, liliongozwa na Polisi Kata wa Somanda, Mkaguzi wa Polisi Mwinjuma Omary, ambapo wawakilishi wa kikundi hicho walifanya jogging hiyo kabla ya kuelekea hospitalini kuwatembelea wagonjwa.



Katika ziara hiyo ya kijamii, wanachama wa Usalama Kwanza Jogging Club waliwajulia hali wagonjwa, kuwapa faraja na kukabidhi msaada mbalimbali kwa wagonjwa wenye uhitaji.





Madaktari na uongozi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji Bariadi waliwashukuru wanachama wa kikundi hicho kwa moyo wa kujitolea na kuonyesha upendo kwa wagonjwa, wakieleza kuwa matendo kama hayo yana mchango mkubwa katika kuwapa wagonjwa faraja na kuongeza ushirikiano kati ya hospitali na jamii.



Kwa upande wao, baadhi ya wagonjwa walionufaika na msaada huo waliwashukuru wawakilishi wa Usalama Kwanza Jogging Club wakiongozwa na Polisi Kata wa Somanda, Mkaguzi wa Polisi Mwinjuma Omary, kwa kuwajali na kuwapa moyo katika kipindi chao cha matibabu.



Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Mkaguzi wa Polisi Mwinjuma Omary alisema kuwa kikundi hicho kitaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki mazoezi kwa ajili ya kujenga afya bora, sambamba na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii zenye manufaa kwa wananchi.



Usalama Kwanza Jogging Club, kupitia kaulimbiu yake “Kata Wese, Afya ni Mtaji,” inaendelea kuhamasisha jamii kuzingatia afya, mazoezi na mshikamano kwa kusaidiana katika nyakati mbalimbali.

Mwisho .

Na mpiga  picha wetu khan kilunga 












Post a Comment

0 Comments