Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

🕯TANZANIA YAOMBOLEZA: MAMA MZAZI WA HAYATI MAGUFULI AMEFARIKI DUNIA.

 


Na mwandishi wetu 

Mama mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Bi. Suzana Magufuli amefariki dunia leo Mei 25, 2026 mjini Chato, mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu.


Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wa Hayati Dk. Magufuli, Jesca Magufuli, kupitia mazungumzo ya simu na AyoTV, ambapo amesema kuwa Bi. Suzana amefariki majira ya saa 1 usiku nyumbani kwake Chato.


“Bibi yetu (Suzana Mussa) amefariki saa moja nyumbani kwake Chato baada ya kuugua kwa muda mrefu. Taratibu za msiba familia itawajulisha. Bwana ametoa na Bwana ametwaa,” amesema Jesca Magufuli.


Familia inaendelea na maandalizi ya msiba huku taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mazishi zikitarajiwa kutolewa baadaye.



Tunatoa pole kwa familia ya Hayati Dk. Magufuli pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments