Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

WIZI WA BETRI ZA CT-SCAN NYAUMATA, POLISI WAKAMATA WATATU.



Na marykitoto 

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limefanikiwa kuwakamata watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa betri za mashine maalumu ya uchunguzi wa magonjwa kwa kutumia mionzi (CT-SCAN) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Nyaumata.


Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, mahojiano ya kina yanaendelea kwa lengo la kubaini zaidi kuhusiana na wizi wa betri hizo pamoja na swichi ya kubadili umeme.


Aidha, Jeshi la Polisi limeonya watu wanaojihusisha na vitendo vya kuhujumu miundombinu ya huduma za afya, likiwataka kuacha mara moja vitendo hivyo vinavyokwamisha juhudi za Serikali za kuboresha huduma kwa wananchi.


Jeshi hilo pia limewaonya watu wanaojipatia kipato kwa njia zisizo halali, hususan wanaonunua au kuuza vifaa vinavyotokana na wizi, na kusisitiza umuhimu wa kujiepusha na vitendo hivyo vinavyokiuka sheria.


Tukio hilo linaibua umuhimu wa kulinda miundombinu ya afya ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma muhimu za matibabu bila vikwazo.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments