Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

AJALI MBAYA MOROGORO: BASI LA ABIRIA NA LORI LA MBAO ZAGONGANA NA KUTEKETEA KWA MOTO




Na kitoto Digital, Morogoro

Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mbao katika eneo la Mkambalani, Wilaya ya Morogoro, mkoani Morogoro. Magari hayo yanadaiwa kuteketea kwa moto muda mfupi baada ya ajali hiyo.

Ajali hiyo imetokea katika barabara kuu ya Morogoro–Dar es Salaam, huku taarifa za awali zikieleza kuwa baadhi ya watu waliokuwa ndani ya magari hayo wamefariki dunia na wengine huenda wamejeruhiwa.

Katika tukio jingine, ajali imeripotiwa kutokea usiku katika eneo la Dakawa, Mkambarani, kwenye barabara kuu ya Morogoro–Dodoma, ambapo basi na lori vinadaiwa kugongana na kuteketea kwa moto.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha huku wengine wakiripotiwa kujeruhiwa. Shughuli za uokoaji zinaendelea, ingawa idadi kamili ya waliofariki na waliojeruhiwa bado haijathibitishwa rasmi.

Aidha, taarifa nyingine zinaeleza kuhusu ajali inayodaiwa kuhusisha gari la Polisi na gari jingine ndani ya Halmashauri ya Morogoro.

Hata hivyo, hadi sasa maelezo zaidi kuhusu mazingira ya ajali hiyo, idadi ya wahusika na hali zao hayajafahamika.

Kitoto Digital inaendelea kufuatilia matukio hayo ili kuwafikishia wasomaji taarifa sahihi na zilizothibitishwa kutoka kwa mamlaka husika.

Taarifa rasmi kuhusu idadi ya waliofariki, waliojeruhiwa na chanzo cha ajali hizo zinatarajiwa kutolewa baada ya uchunguzi na uthibitisho wa mamlaka husika.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments